Ufuatiliaji wa Utafiti wa EAAMO'21

Wito wa ushiriki

Tarehe ya mwisho: 14 Juni, 2021

Tarehe: Oktoba 5-9, 2021

Kiunga cha Kuwasilishia: EasyChair

Kongamano la uzinduzi wa Usawa na Ufikiaji katika Mifumo, Taratibu, na Uratibu (EAAMO ‘21) utafanyika mnamo tarehe 5-9 mwezi Oktoba, 2021, kupitia mtandao, kwenye Zoom na Gather.town.

Lengo la tukio hili ni kuangazia kazi ambapo mbinu kutoka kwenye mifumo, taratibu na uratibu wa hesabu za biashara, pamoja na ufahamu kutoka kwenye sayansi ya kijamii na masomo ya kibinadamu, inaweza kuboresha ufikiaji wa fursa kwa jamii ambazo hazikustahili kihistoria na jamii zenye shida.

Kongamano hilo linakusudia kukuza jamii anuwai, kuwezesha muingiliano kati ya wasomi, tasnia, na sekta za umma na za hiari. Ili kutekeleza hili, inachukua mtazamo mpana wa namna utafiti unavyoweza kuchangia upatikanaji wa fursa, na unakaribisha kazi kutoka kwenye hatua zote za utafiti kuingia kwenye vitendo. Hii pia inahusisha kazi ambayo inaangazia ufahamu wa kawaida juu ya utendaji kazi wa mifumo ya kijamii. Programu hiyo itaangazia uwasilishaji muhimu kutoka kwa watafiti na watendaji na pia michango ya uwasilishaji katika utafiti, sera na utendaji.

Tunaomba mawasilisho katika ufuatiliaji wa utafiti na ufuatiliaji wa sera na utendaji. Mawasilisho yanaweza kujumuisha utafiti, dodoso, na nyaraka za lengo lililotakiwa na pia mawasilisho yanayochagizwa na matatizo na utendaji kutoka kwa wasomi kutoka kwenye nyanja yoyote na watendaji kutoka kwenye sekta yoyote.

Tunahimiza mawasilisho kutoka kwenye taaluma za aina mbalimbali na ukigusia maeneo yanayohusisha ushiriki wa raia, data za uchumi, ubaguzi na upendeleo, ukosefu wa usawa wa kiuchumi, maendeleo ya kiuchumi, elimu, mazingira na hali ya hewa, huduma za afya, nyumba, masoko ya kazi, na sheria na sera. Nyaraka zitapitiwa na wataalamu wenza katika eneo husika la kitaaluma. Mwisho wa mawasilisho ni tarehe 14 Juni, 2021.

ACM EAAMO ni sehemu ya mpango wa Kubuni Utaratibu kwa Faida ya Jamii (MD4SG), na unaunda kwenye mifululizo ya semina za mafunzo ya kiufundi ya MD4SG na semina za ukufunzi kwenye mikutano ikiwa ni pamoja na ACM EC, ACM COMPASS, ACM FAccT, na WINE.

Aina za Uwasilishaji

Mawasilisho yatatarajiwa katika moja kati ya vipengele viwili:

Kwa mawasilisho yote katika ufuatiliaji wowote, mada za kuzungumziwa zinajumuisha lakini hazizuiliki kwenye:

  • changamoto za muundo wa soko na utaratibu katika mazingira yenye rasilimali chache
  • mifumo ya ugawaji ili kuboresha upatikanaji wa fursa
  • kuboresha utoaji wa huduma za kijamii na tathmini
  • kutenga fedha za bima ya afya na kusimamia upatikanaji wa huduma za afya
  • utoaji sawa wa huduma za afya katika jamii zote
  • ukosefu wa usawa wa kiuchumi na uhamaji wa makazi kizazi na kizazi
  • kupunguza matokeo ya uchumi yasiyolingana katika masoko ya kazi ya kwenye soko na nje ya soko
  • kugundua uwepo au sababu za tabia ya kinyonyaji ya soko katika masoko ya kazi
  • kuboresha utofauti na usawa kwa kutumia njia za kimfumo
  • kanuni za soko kwa ajili ya data na faragha
  • kutathmini athari za walimu, shule, au sera ya elimu
  • kuboresha ugawaji wa rasilimali za kielimu
  • kupima na kutathmini maendeleo kufikia malengo ya maendeleo endelevu
  • kupunguza udororaji katika mashamba ya wakulima wadogo na usimamizi wa usambazaji wa rasilimali duni
  • mapendekezo ya kimfumo kuhimiza ushiriki wa raia
  • kutathmini usawa katika uwakilishi wa uchaguzi
  • kutoa taarifa ya mabadiliko ya hali ya hewa na muundo wa sera
  • kubuni mifumo sawa ya usafirishaji
  • kukabiliana na changamoto za miundombinu zinazoathiri jamii zilizotengwa
  • kuzingatia maadili wakati wa kutumia hatua zinazotaarifiwa na mfumo na muundo wa utaratibu katika mipangilio ya sekta ya umma

Ufuatiliaji wa Utafiti

Mawasilisho kwenye ufuatiliaji wa utafiti yanaweza kuanzisha nadharia mpya au matumizi au inaweza kuwa nyaraka za kufikia yaliyokusudiwa zinazojumuisha kazi zilizopo na mitazamo au kuonyesha mielekeo wa siku zijazo. Mawasilisho yatatarajiwa katika moja ya maeneo matano yaliyolengwa:

  • Mfumo wa Akili ya Utambuzi wa Kutengenezwa (AI) na Kujifunza kwa Mashine ikiwa ni pamoja na AI ya athari ya kijamii, hoja ya kitakwimu na upendeleo wa uwezekano wa jambo kutokea, sayansi ya data, upendeleo na ufikiriaji wa usawa, mgawanyo wa haki na ugawaji wa rasilimali, muingiliano wa kompyuta na binadamu katika mifumo ya kijamii na kiufundi, mifumo ya mawakala wa aina mbalimbali, faragha na usalama, na chaguo la nadharia ya kijamii.
  • Mifano Iliyotumiwa na ile ya Upimaji ikiwa inahusisha na kupendekeza na kuchambua mifano iliyotumiwa ya matatizo kwa vitendo vya eneo husika katika AI kwa athari za kijamii, sayansi ya data, soko na muundo wa utaratibu, nadharia ya uchumi mdogo, usimamizi wa usambazaji, sayansi ya kijamii ya hesabu, mawakala wa aina mbalimbali wa uchumi na mawakala wa aina mbalimbali wa mifumo.
  • Mafunzo ya Uhalisia ikiwa ni pamoja na uchambuzi wa uhalisia wa sera za ulimwengu, mifumo, na utaratibu, tafiti za upimaji, matumizi ya uchumi mdogo uliopo, shirika la viwanda asilia, tafiti na njia za majaribio, masomo ya eneo husika, kujifunza mashine, uthibitisho wa sababu, na sayansi ya kijamii ya kihesabu.
  • Nyaraka za Muelekeo wa Utafiti zinazoangazia mada au uwanja fulani wa utafiti na kuleta dhana mpya ya mada iliyojadiliwa. Mawasilisho haya yatalenga kuwasilisha msimamo wa masuala kadhaa, wazo, au kufungua eneo jipya la majadiliano juu ya mada fulani ya utafiti inayohusiana na wigo wa mkutano. Mawasilisho yatatathminiwa kulingana na uhusika wao na uwezo wa kutoa kanuni mpya za kuandaa ufanyaji kazi, kukuza mitazamo mipya na kuwa ni kama madaraja kati ya utafiti na sera/utendaji kazi.
  • Nadharia ikiwa ni pamoja na uchambuzi wa kinadharia katika muundo wa mfumo, mgawanyo wa haki na ugawaji wa rasilimali, nadharia ya mchezo, muundo wa soko na mpangilio wa utendaji kazi, mifumo ya kitabia, uboreshaji, usimamizi wa shughuli, uchaguzi wa kijamii wa kihesabu, uchambuzi wa mtandao wa kijamii, na nadharia ya kujifunza mashine.

Maelekezo ya Uwasilishaji

Kwa ufuatiliaji wa utafiti, mawasilisho yatakuwa na chaguo la kuwa ni ya kumbukumbu au isio ya kumbukumbu, na upendeleo uliopewa kuwa nyaraka za kumbukumbu. Ufuatiliaji wa kumbukumbu unakaribisha mawasilisho ambayo yanajumuisha nyaraka mpya za utafiti ambazo hazijachapishwa katika maendelezi za kongamano hapo awali. Ufuatiliaji wa kumbukumbu unakaribisha nyaraka ambazo ziko kwenye utaratibu wa kuchapishwa kwenye majarida. Ufuatiliaji ambao sio wa kumbukumbu pia unakaribisha nyaraka za utafiti ambazo hazijachapishwa mapema kuzidi mwezi Januari mwaka 2019. Waandishi wanapaswa kupakia PDF ya utafiti wao kwenye EasyChair. Hakuna mahitaji ya upangiliaji au urefu wa uwasilishaji wa nyaraka ya mfumo wa PDF, lakini nyaraka zilizokubalika zitakuwa na kikomo cha kurasa 10 wakati wa kuchapishwa. Mbali na mfumo wa PDF, waandishi wanatakiwa kupakia maelezo yenye maneno 200-250 kwenye EasyChair kwa muhtasari wa kile walichokiwasilisha na umuhimu wake kwenye kongamano hilo.

Mawasilisho yanafanywa bila ya kujua ni nani ambaye amehusika nayo: waandishi wanapaswa kuchukua tahadhari wasijumuishe majina na ushirika wa waandishi kwenye karatasi zao, pamoja na wakati wa kutaja kazi ya awali. Wawasilishaji wanapaswa kuorodhesha waandishi wote wenza juu ya kazi iliyowasilishwa katika EasyChair lakini sio kwenye mfumo wa PDF ya uwasilishaji.

Kutakuwa na chaguo la kuchagua kati ya kutunza kumbukumbu (kwa zile zilizochapishwa) au zisizo za kumbukumbu (ambazo hazikuchapishwa). Waandishi wanaweza kuwasilisha kazi ambazo hazijachapishwa, kazi inayopitiwa kabla ya kuwasilishwa, au kazi ambayo imechapishwa mapema zaidi ya Januari ya mwaka 2019. Ikiwa kazi hiyo tayari imechapishwa, tafadhali jumuisha nukuu kwenye EasyChair.

Tutakubali tu mawasilisho kwa lugha ya Kiingereza. MD4SG na EEAMO wamejitolea kwa kukuza jamii za lugha nyingi, na tunatarajia kuruhusu mawasilisho katika lugha zingine kwenye matukio yajayo.

Mapitio

Mawasilisho yatafanyiwa tathmini kwa kuzingatia vigezo hivi vifuatavyo:

  • Ubora wa uwasilishaji unaopimwa kwa usahihi na uwazi wa ufafanuzi.
  • Umuhimu kwa lengo la kongamano.
  • Uwasilishaji wa tukio jipya na halisi linalowezekana: tunahimiza sana kazi ambayo inachunguza matumizi ya tukio halisi linalowezekana au hutumia mbinu za matendo mapya yanayowezekana kusoma matukio ya programu zilizopo.
  • Pia, mawasilisho yatatathminiwa kulingana na:
    • Uwezo wa kazi ya ufuatiliaji wa taaluma mbalimbali. Tunakaribisha mawasilisho yenye uwezo wa kuchochea ushirikiano kati ya taaluma mbalimbali,
    • Uwasilishaji wa maarifa maalum ya eneo. Tunakaribisha haswa watendaji walio na hamu au uzoefu katika kutafsiri kati ya shida za kiutendaji na njia za utafiti wa kitaaluma.

Nyaraka ambazo ziko nje ya mtazamo wa kongamano kama zilivyotathminiwa na vigezo hivi zinaweza kukataliwa kushiriki.

EAAMO’21 itafuata mfumo wa ukaguzi wa awamu mbili. Mawasilisho yote yatakaguliwa na watu wa kada moja ambapo ni angalau wahakiki 2 katika muundo wa kutojua wanahakiki kazi ya nani hasa. Kamati ina haki ya kutopitia maelezo yote ya kiufundi ya maoni ya mawasilisho.

Jisajili hapa kushiriki kwenye kongamano. Kongamano hilo litatoa msaada wa kifedha kwa gharama za usajili, pamoja na mipango ya taarifa. Maombi yote ya msaada wa kifedha lazima yawasilishwe ifikapo tarehe 14 Juni, 2021 saa 11 jioni ET; maombi yaliyopokelewa baada ya tarehe hii hayatazingatiwa.

Taarifa za muhimu

  • Tarehe ya Mwisho ya Kuwasilisha Utafiti: 14 Juni, 2021
  • Ukurasa wa Kuwasilishia Utafiti: EasyChair
  • Tarehe ya mwisho wa Maombi ya Msaada wa Kifedha: 14 Juni, 2021 saa 11 jioni (saa tatu usiku GMT)
  • Siku ya Kujulishwa: 12 15 Agosti, 2021
  • Tarehe za Tukio: 5-9 Oktoba, 2021